Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akizungumza na waandishi wa habari jijini Nairobi, Kenya.
UNEP/Duncan Moore

Afrika inaweza kuwa jabalí la nishati jadidifu- Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aliyeko Nairobi Kenya kushiriki mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mashirika yasiyo ya kiserikali, UNCSC amezungumza na waandishi wa habari ambapo pamoja na mambo mengine amesema wakati huu ambapo bara la Afrika linakabiliwa na madhara ya mabadiliko ya tabianchi, bara hilo linaweza kuwa jabalí wa uzalishaji nishati jadidifu duniani iwapo litawezeshwa.

Sauti
9'43"
Washiriki wakikusanyika katika ufunguzi wa mkutano wa Umoja wa Mataifa wa asasi za kiraia, unaofanyika katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa jijini Nairobi, Kenya, kuanzia tarehe 9-10 Mei 2024.
UN Nairobi

Mkutano huu wa asasi za kiraia ni muhimu kwa ajili mustakbali ujao: UN

Leo mkutano wa Umoja wa Mataifa wa asasi za kiraia umeng’oa nanga ukiwaleta pamoja washiriki zaidinya 3000 kutoka kila kona ya dunia wakijumuisha wawakilishi kutoka asasi za kiraia, serikali, maafisa wa Umoja wa Mataifa, vijana waleta mabadiliko, wanazuoni, wadau wengine na vyombo vya habari wakifanya majadiliano ya awali na kutoa takwimu kuelekea mkutano wa wakati ujao utakaofanyika New York Marekani mwezi Septemba mwaka huu.