Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UN News

Ally Mwamzola: Vijana tushiriki kuanzia kuandaa hadi kutekeleza ‘Mkataba wa siku zijazo’

Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa asasi za kiraia (UNCSC) ukitamatika leo, miongoni mwa waliohudhuria ni Ally Mwamzola kutoka Asasi ya Umoja wa Mataifa Tanzania (UNA Tanzania). Yeye akiwa anapeperusha bendera ya vijana kwa kuzingatia kuwa pia ni Mratibu wa Mradi wa Ujumbe wa Vijana wa Afrika kwenda Umoja wa Mataifa anayataja mambo matatu ambayo katika mkutano huu vijana walikuwa wanayalenga zaidi. Amezungumza na Stella Vuzo Afisa Habari wa Kitengo cha mawasiliano cha Umoja wa Mataifa, UNIS nchini Kenya na anaanza kwa kumweleza waliyowasilisha.

Sauti
3'6"
UN News

Vijana wakiwezeshwa wanaweza kuinua uchumi na kusongesha agenda ya SDGs - Zahra Salehe

Mnamo tarehe Mosi Januari mwaka 2016, Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (SDGs) yalianza kufanyiwa kazi rasmi. Tangu wakati huo watu ulimwenguni kote kwa ngazi tofautifauti wamekuwa wakihaha kuhakikisha kufikia mwaka 2030 malengo hayo yanafikiwa. Na kila mara Makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani yamekuwa uwanja wa wazi kwa wadau kutoka kila pembe ya dunia kuja katika mikutano mbalimbali na kubadilishana uzoefu.

Sauti
5'17"
UN News/Anold Kayanda

Hatuna uhakika wa kuitimiza SDG5 kwa 100% lakini tunaweza kufikia hata 90% - Abeida Rashid Abdallah

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, nchini Tanzania, Abeida Rashid Abdallah hivi karibuni akiwa katika safari ya kikazi kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, Marekani kushiriki vikao vya mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW68 anajibu swali aliloulizwa na Anold Kayanda wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa kwamba Je, Lengo namba 5 la Maendeleo Endelevu linalohamasisha usawa wa kijinsia litafikiwa huko Zanzibar kufikia mwaka 2030?

Sauti
3'28"
© UNHCR/Mohamed Maalim

UNHCR inawasaidia wakimbizi dhidi ya mafuriko Afrika Mashariki

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi, UNHCR, linapambana kuhakikisha linawasaidia wakimbizi katika maeneo mbalimbali ya ukanda wa Afrika Mashariki dhidi ya madhila yanayosababishwa na mafuriko makubwa kutoka na mvua za El Niño zinazoendelea. Makala hii ambayo video zake zimekusanywa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR inaanzia Bujumbura Burundi kisha inakupeleka Kenya katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab, kama inavyosimuliwa na Evarist Mapesa.

Sauti
3'13"
© UNICEF/UN0323295/Frank Dejongh

Mabadiliko ya tabianchi yamefanya urembo wa Kimaasai Kenya kuwa mbadala wa kujikimu kimaisha: Samante Anne

Mabadiliko ya tabianchi yamekuwa mwiba kwa jamii nyingi yakizilazimu kubadili mfumo wao wa Maisha ili kukabiliana na athari zake kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. Miongoni mwa jamii zilizoathirika na janga hilo ni za watu wa asili wakiwemo Wamaasai kutoka Kenya na hususan wanawake. Je wanahimili vipi athari hizo? Flora Nducha alipata fursa ya kuzungumza na mmoja wa wanawake wa jamii hizo za Wamaasai aliyekuwa New York hivi karibuni kushiriki jukwaa la watu wa jamii za asili Bi.

Audio Duration
2'49"
UNCDF

Wanawake Tanzania wainua wanawake wenzao katika ujasiriamali kupitia mradi wa CookFund

Nchini Tanzania mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuendeleza mitaji, UNCDF uitwao CookFund unaofadhiliwa na Muungano wa Ulaya umesaidia wajasiriamali hasa wanawake kuinua wanawake wenzao kwenye sekta ya matumizi ya nishati jadidifu na hivyo kutekeleza ajenda ya 2030 ya Umoja wa Mataifa ya sio tu kuondokana na umaskini bali pia kuhimili na kukabili mabadiliko ya tabianchi.

Sauti
3'37"
Mathias Tooko

Mabadiliko ya tabianchi yanachangia katika migogoro katika jamii za asili - Alois Porokwa

Mkutano wa 23 wa Jukwaa la Kudumu kuhusu Masuala ya Watu wa Asili, UNPFII uliodumu kwa wiki mbili hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa umefikia tamati leo Aprili 26. Miongoni mwa masuala muhimu yaliyojadiliwa ni mabadiliko ya tabianchi na mazingira, likiwa ni suala ambalo pia miezi miwili iliyopita lilipewa kipaumbele cha juu wakati wa Mkutano wa 6 wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEA 6  jijini Nairobi, Kenya.

Sauti
4'3"
UN /Andi Gitow

Jamii za watu wa asili wanaathiriwa pakubwa na mabadiliko ya tabianchi - Samante Anne

Hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa Mkutano wa 23 wa Jukwaa la Kudumu kuhusu Masuala ya Watu wa Asili, UNPFII ukielekea ukingoni huku mambo kadha yakiwa yamejadiliwa kwa wiki mbili na miongoni mwa mambo hayo ni suala la mabadiliko ya tabianchi na mazingira, nilipata fursa ya kuzungumza na mmoja wa washiriki wa jukwaa hilo Samante Anne kutoka shirika lisilo la kiserikali nchini Kenya la Mainyoito Pastoralists Intergrated Development Organization (MPIDO) akieleza namna mabadiliko ya tabianchi yalivyoathiri jamii za watu wa asili nchini mwake.

Sauti
4'44"
UNICEF TANZANIA

Watoa chanjo wavuka mabonde na mito kufikisha chanjo kwa walengwa Tanzania

Wiki ya kimataifa ya chanjo ikifungua pazia, nchini Tanzania wahudumu wa afya kama Prisca Mkungwa wanajitoa kwa kadri ya uwezo wao kuhakikisha huduma za chanjo zinafikia walengwa wote hata wale walioko maeneo ya mbali. Mathalani huko wilayani Chunya, mkoani Mbeya, kusini magharibi mwa taifa hilo ambako kupitia ushirikiano na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, chanjo dhidi ya surua inatolewa kwa watoto.

Sauti
3'32"